BBA The Chase: Baada ya kutolewa Betty akutana na vikwazo nchini kwake Ethiopia, hatarini kushitakiwa kwa “kufanya mapenzi hadharani” na Bolt!
Mtandao mmoja wa Ethiopia
umeripoti kuwa aliyekuwa
mshiriki wa nchi hiyo katika
BBA ‘The Chase’ Betty Abera
yuko hatarini kufunguliwa
mashitaka kwa “kufanya
mapenzi hadharani” na mpenzi
wake Bolt katika reality show
hiyo inayoendelea huko Afrika
Kusini.
Kwa mujibu wa mtandao wa
Awramba Times wa Ethiopia,
kikundi cha wanasheria wa
Addis Ababa wamekamilisha
maandalizi ya kumshitaki
mshiriki huyo wa BBA ambaye
tayari ameshauaga mchezo,
kwa “kufanya mapenzi
hadharani” kinyume cha sheria
za nchi hiyo ambazo haziruhusu
watu kufanya tendo hilo
hadharani.
Kwa mujibu wa radio moja ya
Addis Ababa, endapo Betty
atakutwa na hatia kuna
uwezekano akatumikia kifungo
cha miaka 6 nyuma ya nondo
(jela).
Inaaminika kuwa Bolt na Betty
ndio walikuwa couple ya
kwanza kufanya tendo hilo
katika The Chase, kitu
kilichoshuhudiwa na watazamaji
wengi kutoka nchi mbalimbali
za Africa .
Baadhi ya watu wa Ethiopia
wametoa maoni yao kwa
kuonesha udhaifu wa tuhuma
hizo kutokana na sababu
kadhaa za msingi zikiwemo:
1.Betty hajafanya tendo hilo
mbele za watu (public) kama
inavyodaiwa kwasababu
hapakuwa na mtu zaidi ya
camera wakati tukio hilo
likifanyika
2. Hakuna uthibitisho kama
kweli walifanya tendo hilo
sababu walikuwa wamejifunika
blanketi
3. Tukio hilo halijafanyika ndani
ya Ethiopia hivyo haina nguvu
kwasababu sheria hiyo inafanya
kazi ndani ya mipaka ya
Ethiopia.
4. Serikali ya Ethiopia inapaswa
kukishitaki kituo cha TV (DSTV)
kilichorusha content hiyo kwa
watazamaji wa Ethiopia na sio
kumshitaki Betty.
No comments:
Post a Comment