Rapper Babu Sikare aka Albino
Fulani aishiye nchini Marekani
ameiambia Bongo5 kuwa
amesikitishwa na jinsi wasanii
wengi wa Tanzania
walivyoshindwa kujitokeza na
kumpongeza Wakazi kwa
performance kali aliyoitoa jana
kwenye eviction show ya Big
Brother Africa The Chase.
“Nilikuwa na matarajio
makubwa zaidi, kwamba
wasanii wakubwa watajitokeza
na kuwa proud ya young new
talent. Kabla kuna waliokandya,
he did good na hapati credit
stahili,” amesema Sikare.
Hata hivyo amekiri kuwa sio
wote huiona show hiyo
kwakuwa huonekana kwa wale
walio na DSTV lakini
amesisitiza, “Ila pia nimeona
ma artist wakubwa wakibishana
na kuonyesha kuwa ni wapemzi
damu wa BBA. Basi hata
kusema “hongera, nimesikia….”
“Kuna nyufa katika sanaa yetu.
Ili tuendelee inabidi tuwe na
ushirikiano ndani na nje ya
studio tunapokutana. Tusijenge
mioyo yenye Chuki, Wivu,
kinyongo kati ya wasanii na
wasanii. Ndio maana unasikia
fulani karushiwa chupa kwa
steji…. Tukiendelea namna hii
kutakuwa na Makundi
yatakayoua sanaa.”
Uncategories
Albino Fulani: Nilitarajia
wasanii wengi Tanzania
wangempongeza Wakazi
kwa kazi nzuri ya jana
kwenye BBA Eviction
Show
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment