Breaking News
recent

Mwanawe Pele jela miaka 33

Edinhio Pele alikuwa mlinda lango
kabla ya kusataafu soka
Mwanawe gwiji wa soka Brazil
na duniani kote, Pele, Edinho
Pele, amefungwa jela miaka 33
kwa kufanya biashara haramu
ya pesa au kujipatia pesa chafu
zilizotokana na biashara ya
ulanguzi wa dawa za kulevya.
Edinho ni mchezaji soka mstaafu,
aliyecheza kama mlinda lango
katika klabu ya Santon aliyowahi
kuchezea Pele mapema miaka ya
tisini.
Alikamatwa kwa mara ya kwanza
mwaka 2005 na kutumikia kifungo
kwa kosa la ulanguzi wa dawa za
kulevya pamoja na kuwa na
uhusiano na mlanguzi sugu wa
dawa hizo mjini Santos.
Edinhio, alikiri kosa la kuwa
mraibu wa dawa za kulevya lakini
alikanusha madai ya kuhusika na
ulanguzi wa dawa hizo.
Uamuzi wa mahakama ulitolewa
mjini Praia Grande, katika jimbo
la Sao Paulo.
Vyombo vya habari nchini humo
bado havijaweza kupata kunena
na Edinho, ambaye jina lake halisi
ni Edson Cholbi do Nascimento,
lakini vinasema kuwa huenda
akakata rufaa.
Pele alimtembelea mwanawe Jela
Edinho, mwenye umri wa miaka
43, alikuwa mlinda lango wa
Santos.
Pele, au kwa jina lengine, Edson
Arantes do Nascimento, alisakatia
soka yake nchini Brazil , na
kuwakilisha Brazil katika kombe la
dunia mwaka 1958, 1962 na 1970
na kupata sifa ya kuwa mchezaji
bora katika kizazi chake.
Pele mwenye umri wa miaka 73,
alishinda kombe la dunia mara
tatu akichezea Brazil na kuingiza
zaidi ya mabao 1,200 katika
historia yake ya kucheza.
Alistaafu mwaka 1974, lakini
akaanza kucheza tena mwaka
mmoja baadaye mjini New York
Marekani.
Edinho ni mtoto wa tatu wa Pele
kutoka kwa ndoa yake ya kwanza.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.