Breaking News
recent

Instagram yafuta picha za Uchi

Kevin Systrom afisaa mkuu
mtendaji wa Instagram
Mmoja wa waasisi wa mtandao
wa kijamii wa Instagram,
ameambia BBC kuwa sheria
zake kuhusu picha za uchi
hazimbagui mtu yeyote.
Kampuni hiyo imekosolewa vikali
kwa kwa kuondoa picha za
wanawake walio nusu uchi kwenye
mtandao huo.
Lakini Afisaa mkuu mtendaji wa
mtandao huo wa kijamii, Kevin
Systrom, amesema kuwa sheria
hizo zinalenga kuhakikisha kuwa
vijana na watu wazima
wanaotumia mtandao huo wako
salama.
Masharti ya matumizi ya mtandao
wenyewe, yanasema: 'Mtu
haruhusiwi kuweka picha za watu
walio nusu uchi na picha zenye
mada ya ngono. ''
Matamshi yake yanakuja baada ya
mwanawe muigizaji maarufu,
Bruce Willis, Scout Willis kuweka
picha yake kwenye mtandao huo
akiwa nusu uchi bila kitu kifuani.
Picha hiyo iliondolewa kwenye
mtandao huo na wamiliki wa
mtandao na hapo ndipo
malalamiko yalianza kuibuka.
Muimbaji Rihanna, ambaye
alikuwa na wafuasi milioni 1.3
aliunga mkono kampeini hiyo
kabla ya kufunga akaunti yake.
Wamiliki wa mtandao huo
wanasema sheria zinapaswa
kufuatwa na kila mtu awe mtu
mashuhuri au vinginevyo.
"lengo letu ni kuhakikisha kuwa
Instagram, ni mahala salama kwa
kila mtu , awe maarufu au la. ''
"tunapaswa kuwa na sheria na
kuhakikisha kuwa kila mtu
anafuata sheria hizo. Bila shaka
tunapata changamoto nyingi
lakini tutnaedneklea kusisitiza
umuhimu wa sheria kufuatwa, ''
alisema Systrom
Huku umaarufu wa mtandao huo
ukiendelea kuimarika, mtandao
huo umekosolewa kuhusiana na
baadhi ya picha zinazochapishwa
humo . Pia mtandao wenye
umebana baadhi ya maneno
yanayohusiana na madawa ya
kulevya.
Instagram ilinunuliwa na
Facebook mwaka 2012.

ABC

ABC

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.