Luka Podolski na Theo Walcott
wakisherehekea.
Theo Walcott alifunga magoli
mawili naye Luka Podolski
alifunga la tatu na kuisaidia
Arsenal kutoka nyuma na
kuishinda West Ham katika
uwanja wao wa nyumbani na
kurejea tena kileleni mwa ligi
kuu ya Premier.
Arsenal ilitawala kipindi cha
kwanza lakini Carlton Cole
aliifungia West Ham bao lake la
Kwanza baada ya kipa wa Arsenal
Wojciech Szczesny kutema mpira
kwenye eneo la hatari
West Ham ilipoteza nafasi nyingi
za kufunga hali iliyompa Walcott
kusawazisha.
Muda mfupi baadaye Podolski
alimpa Walcott pasi nzuri ambaye
aliitia kimyani na kuiweka Arsenal
mbele kwa magoli mawili kwa
moja.
Kufuatia matokeo hayo West Ham
sasa imeshuka hadi nafasi ya
kumi na saba alama moja tu
mbele ya timu tatu zinazoshikilia
nafasi za mwisho.
Timu hiyo imeshinda mechi moja
tu kati ya mechi kumi na moja
zilizopita na itakuwa na kibarua
kigumu kubadili matokeo hayo
wakati itakapochuana na West
Brom siku ya Jumamosi.
Arsenal sasa inaongoza ligi hiyo
na alama thelathini na tisa alama
moja nyuma ya Manchester City
ambayo iliilaza Liverpool kwa
magoli mawili kwa moja.
Chelsea inashikilia nafasi ya tatu
na alama thelathini na saba
kufuatia ushindi wake wa bao
moja kwa bila dhidi ya Swansea.
ABC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment